JAMAA wawili, mmoja fundi umeme, Rashid
Balazi na Juma Bushiri wanadaiwa kunusurika kifo baada ya kutekwa na kusulubiwa
nyumbani kwa msanii wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu wakituhumiwa
kukwapua simu ya bei mbaya ya mpambe wa mwanadada huyo, Petit Man, Amani
limeichimba kwa kina.
|
PF 3 aliyopewa bwana Rashid Balazi kwa ajili ya kwenda kupata
matibabu.
|
|
Rashid Balazi akiwa na jeraha begani baada ya kutekwa na kupigwa.
|
Walisimulia kwamba, baada ya
kugundua hilo waliomba fedha kwa Bite kwa ajili ya kwenda kununua bomba,
wakapewa shilingi elfu arobaini.“Lakini kabla hatujafika kunakouzwa mabomba
tulipigiwa simu na Bite kwamba tunatakiwa kurudi kwa kuwa kuna tatizo.
|
Baadhi ya majeraha aliyoyapata Juma Bushiri.
|
“Walikuwa wakitumia silaha mbalimbali kama
viwembe, visu na fimbo kisha baadaye walitumwagia maji ya moto. Kimsingi
walitufanya kama vibaka wanavyofanyiwa wakikamatwa.
“Kama hiyo haitoshi, Petit Man aliwaita mabaunsa wawili ambao walitutesa na kutuvua nguo tukabaki kama tulivyozaliwa.
“Kama hiyo haitoshi, Petit Man aliwaita mabaunsa wawili ambao walitutesa na kutuvua nguo tukabaki kama tulivyozaliwa.
“Kipigo kilipozidi majirani
walisikia kelele na kuja kuchungulia ambapo walikimbilia kwa mjumbe wa nyumba
kumi na kumpa taarifa, yeye akaja kutuokoa na kutupeleka polisi huku wakati huo
difenda la polisi nalo likawa limeshafika na kumtia mbaroni Petit Man na baadhi
ya watesaji hao na kwenda kuwasweka mbaroni kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’ lakini wengine walikimbia.”
“Tulirudi na kumkuta Petit Man akiwa na
mlinzi. Petit Man alisema eti sisi tumemuibia simu yake ya bei mbaya aina ya
Iphone 6, hivyo tunatakiwa tuirudishe. “Tulimwambia hatukuchukua simu lakini
akasisitiza ni sisi, akasema tutairudisha tutake tusitake.
“Tulipoona tumevaa msala wa uongo
tulimwambia atupeleke polisi, akasema atawaita makamanda wake ambao ni ‘mbwa
mwitu’ waje watuoneshe kazi. Lakini kabla ya kuwaita makamanda wake, alimwita
mganga wa kienyeji. “Mganga alifika akaangalia kwa darubini zake akasema
simu hatujaiba sisi, lakini Petit Man hakutaka kumwelewa.
“Wakati huo alikuwa bado ametufungia ndani
tusitoke, ghafla wakafika hao makamanda wake, hatukuwahesabu lakini walikuwa
wengi, wakatuteka na kutufunga kabla ya kuanza kutusulubisha wakidai wao ni
‘mbwa mwitu’. Jamaa walitupiga kipigo cha mbwa mwizi....”![]() |
| Msanii wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu. |
“Wakati zogo hilo linaanza, Wema
alitoka na kumwambia Petit wawahi uwanja wa ndege (Julius Nyerere, Dar) kwani
walikuwa na safari (walikuwa wanakwenda nchini Ghana).
“Wema na Petit Man waliondoka na kuamuru kwamba tuwasubiri hapohapo tusiondoke.”
“Wema na Petit Man waliondoka na kuamuru kwamba tuwasubiri hapohapo tusiondoke.”
“Walipofika uwanja wa ndege wakawa
wamechelewa ndege, Wema hakurudi nyumbani ila Petit Man alirudi ndipo
tukaanza kupigwa kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 9:00 alasiri,” walieleza
jamaa hao wakiwa hoi kwa kipigo cha shetani.
Katika
tukio hilo, Juma alipata majeraha kibao mwilini ambapo anatembea na mkongojo
huku Rashid akiwa amechanwa na kisu mgongoni, mguuni na mbavu moja ikiwa
imepata ufa na wote hao walipelekwa kwenye Hospitali ya Sinza-Palestina,
Dar.Baadaye Rashid alihamishiwa Mwananyamala kufuatia hali yake kuwa mbaya.
Hata hivyo, washitakiwa hao na
walalamikaji walitakiwa kuripoti kituoni hapo Jumatatu iliyopita lakini
walalamikiwa walikiuka amri ya polisi, hawakuonekana kwa madai kwamba
wamesafiri kikazi kwenda nchini Ghana.
Kwa mujibu ya shitaka
lililofunguliwa kituoni hapo, Petit Man anakabiliwa na tuhuma za kudhuru mwili
katika jalada la kesi namba KJN/RB/11250/2014 na KJN/RB/11220/2014 -SHAMBULIO
LA KUDHURU MWILI.
Walalamikaji hao walieleza kwamba
katika kupigwa huko, Juma aliibiwa simu mbili na fedha taslimu shilingi laki
tatu na themanini huku Rashid akiibiwa shilingi laki tatu ambazo alipewa na
mteja wake kwa ajili ya kwenda kununulia vifaa.
Naye
mjumbe wa eneo la tukio, Muharami Seif alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kukiri kuwaokoa jamaa hao wakiwa katika hali mbaya baada ya kupata taarifa
kutoka kwa majirani hivyo Petit Man na Wema wanasubiriwa watue Bongo
kukabiliana na mkono wa sheria.
Na Mwanaharakati.


No comments:
Post a Comment