BARAZA la Mitihani nchini NECTA
limetangaza matokea ya kidato cha pili yaliyofanyika mwaka jana 2014
huku idadi kubwa ya wanafunzi wakiwa wamefaulu na kujiunga kidato cha
tatu, yakipanda kwa asilimia 92.66 ikilinganisha na mwaka 2013 ambapo idadi ya
wanafunzi waliofaulu ilikuwa asilimia 89.34.
Matokeo hayo yametangazwa leo Jijini
Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dkt Charles E
Msonde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo alisema watahiniwa
waliofanya mtihani huo uliofanyika mwezi Novemba mwaka jana ilikuwa 405,204
sawa na asilimia 89.40 Kati ya hao wasichana walikuwa 233,834 sawa na asilimia
51.60 na wavulana walikuwa 219,357 sawa na asilimia 48.40.
Dkt Msonde alisema kati ya
watahiniwa hao waliofaulu na kupata alama na kuweza kuendelea na kidato cha
tatu walikuwa 375,434 Sawa na asilimia 92.6 ya watahiwa wote waliofanya mtihani
huo ambapo wasichana walikuwa 195,328 sawa na asilimia 92.8 na wavulana 180106 sawa
na aslimia 92.69.
Aidha,Dokt Msonde aliwataja
watahiniwa ambao wamepata alama ambazo hawawezi kuendelea na kidato cha Tatu
na itawanalazimu kurudia kidato cha pili walikuwa 29770 kati ya asilimia
7.34.
Vilevile ,Dokta Msonde aliyetaja masomo
waliofanya vizuri wanatahiniwa hao ni ya
Uraia,Historiya,Kiswahili,kingereza,jeografia
Pia Masomo waliofanya vibaya
watahiniwa hao ni ya Hesabu,Kemia,kilimo,Somo la Biashara pamoja na
Biolojia.
Alibanisha kuwa sababu iliofanya
idadi ya wanafunzi mwaka huu kuwa mazuri imetokana na mipango mizuri ya
serikali huku ikizingatia sasa kuwepo na mfumo mpya wa matokea mkubwa sasa na
akawata walimu na wazazi waendeleea kutoa mshikamano kwa walimu.
Matokeo yote ya Kidato cha pili
yatakuwepo kwenye Mtandao wa baraza la Mitiani nchini,tovuti ya Wizara ya Elimu
na Ofisi ya Wazari Mkuu Tamisemi, pamoja na Kwenye shule husika ya Mwanafunzi
anayesoma.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment