Mahakama kuu ya Tanzania katika kikao chake kilichofanyika
mkoani Geita imewatia hatiani na kuwahukumu kunyogwa mpaka kufa, watuhumiwa wa
nne wa mauaji ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi Zawadi Magindu aliyeuwawa mwaka
2008 katika kijiji cha Nyamalulu wilayani.
Kwa kuzingatia ushahidi na utetezi
wa pande zote jaji Joaquine De-mello amesema mahakama imejiridhisha pasipo
kuacha shaka yoyote kuwa watuhumiwa wote wanne walihusika na mauaji ya Bi
Zawadi Magindu katika kijiji cha Nyamalulu wilayani Geita mnamo.................
tarehe 11 mwezi
wa tatu mwaka 2008 usiku.
Kwa mujibu wa mashahidi
waliojitokeza inasemekana mtuhumiwa namba mbili Ndahanya Lumola na mtuhiwa
namba tatu Singu Siantemi ndio waliohusika na upimaji wa mifupa ya marehemu
Zawadi ambapo hutumia wembe na shilingi moja kuweka karibu na mifupa ya Albino
ili kujua kama itavuta kama sumaku na kipimo kingine ni redio ambayo huiweka
karibu na mifupa na ikizimika ndio mifupa hiyo huonekana kuwa na ubora tofauti
na hapo mifupa hiyo huwa haifai na hutupwa.
Mashahidi hao wamesema vipimo hivyo
havina uhalisia wa aina yoyote kwani hakuna binadamu mwenye mifupa inayokuwa na
sumaku.
Aidha jaji De-mello amesema
anashangazwa na kesi zote alizosimamia zinazohusu mauaji ya Albino watuhumiwa
wote wanaofikishwa mahakamani ni wakataji wa mapanga na kuhoji wakataji hao
wanapeleka wapi mifupa hiyo? Na kuwataka wahusika kuhakikisha wanawapata
wanunuzi na watumiaji wa viongo hivyo vya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Watu waliokutwa na hatia ya kufanya
mauaji hayo ni Masalu Kahindi, Ndahanya Lumola, Singu Siyantemi na Nassoro
Saidi ambaye ni mume wa marehemu Zawadi.
Kwa upande wao watu wenye ulemavu wa
ngozi wameipongeza mahakama kwa kutoa hukumu ya haki inayoashiria kuwapa ulinzi
jamii hiyo ya maalbino.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment