MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday 30 May 2015

MBUNGE AZUIA UANDIKISHAJI BVR KAGERA?



. Ni baada ya kutowaletea maendeleo,
. Mradi wa umeme waelekezwa kwa wachache,
. Barabara mbovu wajasriamali, na wagonjwa walalama.
Ni kutokana na wananchi kubainika kiasi kidogo kujitokeza katika halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera, kwenye uandikishaji BVR kanda B kama zilivyotengwa na halmashauri husika, ambapo mtandao huu umejionea wananchi kiduchu katika  kata Karabagaine kilomita 18 kutoka Bukoba mjini.

Katika vituo vya kijiji Kitwe, na Kangabusharo, mtandao huu umetaka kujua sababu ya kuwafanya wananchi waendelee na shughuli zao ili kwenye vituo umeandikishwa watu 8 tangu saa2 asubuhi hadi saa 7 mchana, ikabainika kuwa wanaamini kujiandikisha ni kunufaisha viongozi hasa wakisiasa, hasa kwa kumtaja mbunge.
KANDAYAZIWA BLOG, imejionea ubovu wa barabara yenye urefu wa kilomita 2.5 kutoka Kiziru kuelekea gereza Rwamulumba, ambapo wakaazi wanaamini kuwa wametupiliwa mbali na viongozi wao.
Wameomba TANROADS kuwapa ruksa ya kukarabati barabara hiyo, ili wajinusuru na baadaye gharama yao irudishwe na wakala hao wa barabara mkoani Kagera, kama mwenyekiti wa kijiji na mtendaji Kagabusharo wanavyoeleza.
Mimi mtendaji wa kijiji Kangabusharo Bi Joyce Kayoza, barabara hiyo imekuwa kero kwetu, lakini pia tutafanya mkutano wa kujadili kjinsi ya kupata pesa za kujenga barabara hiyo, fedha ambayo baadaye wataomba TANROAD iwarudhie kwani itakuwa imetokana na nguvu za wananchi.

Mwishoni mwa mwaka jana, aliyekuwa meneja wa TANROADS mkoani Kagera John Kalupare, alieleza kuwa barabara hiyo iko chini ya mamlaka ya chai Bukoba Tea Company Rwabikanshe, ambao waliomba kwa makubaliano na wakala huo taifa, kuwa watakuwa wakiifanyia marekebisho, kwa kigezo kuwa TANROADS ikikarabati unafanyika uharibifu wa majani chai yaliyo pembezoni mwa barabara hiyo.
Hatahivyo muhandisi John Kalupare, aliongeza kuwa baada ya BTC kushindwa kufanya ukarabati huo, wakala huo umeandika barua kwao ili wakubali kubatilisha makubaliano ya zamani ili TANROADS ikarabati barabara yake, ingawaje kwa sasa, wakala huo Kagera umesema unafuatilia jambo hilo kwa karibu. 

Na Mwanaharakati.

No comments: