.
Asema wawaletee wagombea wanaopendwa,
.
Watumiao udini, siasa na ukabila hawafai,
.
Hatosita kusema kama mambo yanakwenda vibaya.
Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Dr Method
Kilaini, ameiambia sautiyamnyonge kuwa, kiongozi anayetakiwa na jamii ndiye anayepaswa
kuchaguliwa na chama kwani wao ndiyo wapiga kura hivyo wasikoseshwe haki
wanayoipendekeza kuwaongoza.
Hatahivyo ametaja sifa za kiongozi kuwa lazima wananchi wamuulize amewafanyia nini kabla, atafanya nini lakini akasema kuwa
wananchi wanakosa elimu ya kutambua kiongozi bora, hivyo sautiyamnyonge ni moja
ya chombo cha kuwasaidia watu hao
Kumekuwa na desturi za kusambaza kauli za ubaguzi na
kusema udini katika siasa, jambo ambalo amesema haiwezekani wakaendelea kutumia
majukwaa kutukana, akisistiza kuwa angeweza angemwapisha mmojammoja ili
akikiuka alaniwe.
Vyama vya siasa kote nchini, vinaendelea na mchakato wa
kuwapata wagombea wa nafasi ya udiwani, ubunge na urais, huku kukiwa katika
mchakato wa kuomba ridhaa kupitia vyama vyao, ili apatikane kiongozi mmoja kila
kata na jimbo kama ambavyo amepatikana mmoja kwenye nafasi ya urais kupitia
CCM.
Katika manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge ni wanane,
ambapo wajumbe wa kata kupitia chama hicho, wamemwambia mbunge anayemaliza muda
wake, kuwa asiangaike kuomba kura, na chama kingempitisha bila kupingwa ili aendelee
kuleta mazuri anayowafanyia.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment