MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 23 July 2015

KAULI YA AMANI YAWASTUA WANA CCM BUKOBA, MWENYEKITI ANUSURU MKUTANO WA MAONI.



. Kuhusu rushwa taasisi za serikali,
. Baadhi wastukia uhalali wamgombea,
. Ashindwa kubainisha sekta alizotaja kuhusika.
Mwenyekiti wa mtaa uswahili Bw Udd Miiluko akituliza wajumbe baada ya kutaka Amani apishe mkutano kwa kuwadanganya.




Katika mkutano wa kwanza wa waomba ridhaa ya kugombea ubunge ndani ya CCM manispaa ya Bukoba, wagombea ubunge wakisimama mbele ya adhara ya kata bilele kuwaomba wanaCCM kumpitisha mmoja kuwania nafasi ya ubunge kupitia chama hicho, ambapo mmoja wa wagombea asema serikali imejaa rushwa katika setka nne muhimu hapa nchini.

Mtia nia huyo Dr Anatoly Aman kati ya watia nia nane wa manispaa ya Bukoba, ameshindwa kuendelea baada ya kuulizwa swali kama alivyosema kuwapo taasisi nne za wala rushwa, mmoja wa wajumbe alitaka azitaje kwa majina ndipo yeye akasema yafuatayo na kuzua taaruki kwa wajumbe wa CCM kata bilele………......................

Sambamba na hilo, amesema kuwa ataleta maendeleo ya ajabu kwa kujenga soko la kisasa, huku akisema kuwa ameleta muwekezaji na ameanza kuweka taa za barabarani katika manispaa ya Bukoba.

Katika mkusanyiko huo wa wajumbe,ewaomba ridhaa 6 wamesimama kujinadi kila mmoja kwa nafasi yake kueleza watafanya nini, ingawa imeonesha kila anayeulizwa kuhusu uliwahi kufanya nini, imekuwa ngumu kupata swali la moja kwa moja na kuwaridhisha wajumbe kama walivyo tarajia majibu.

Kwa upande wake Mjuni Kataraiya, aliyewahi kuwa mbunge katika jimbo hili 1995- 2000, amejittetea kuwa hakuuza jimbo bali alishindwa tu katika uchaguzi, hivyo anawaomba wananchi ili alete maendeeo kwa kipindi alichokaa bila nafasi hiyo amejifunza mengi. 

Na Mwanaharakati.

No comments: