. Imewataka wananchi kutokubali kuchangia fedha ili
kuunganishiwa huduma ya umeme.
Msemaji wa wizara ya nishati na madini Badra Masoud, amesema kuwa serikali haijaweka
mpango wa kuchangisha watu hela kwa ajili ya huduma, afisa wa wizara wala
kulipa fundi wa Tanesco, akiongeza kuwa fedha elekezi inaweza kuhitajika katika
maeneo ambayo hayako kwenye mpango wa wizara kufikisha umeme kwa wakati huo.
Amesema kuwa nchi inakua kwa kasi na serikali imejipanga
kufikisha umeme kila eneo kulingana fedha zinavyopatikana kwa kusisitiza kuwa
kuna lawama kuhusu mgawo wa umeme, ambao amefafanua kuwa saizi haukuna mgawo
ingawaje ubovu wa miundombinu ndiyo husababisha kukosekana kwa umeme kwa wakati
Fulani.
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi duniani na uharibifu wa
vyanzo vya maji, Tanzania inakosa mvua
za kutosha na kusababisha gharama za
umeme kupanda baada ya mabwawa ya Mtera kukauka ambayo huzalisha umeme wa wa
bei nafuu kuliko umeme wa aina yoyote mpaka sasa.
Tanzania ina megawati 1500 za umeme ambazo hutumika kati ya
megawati 800 na 900 nchi nzima kutoka vyanzo vya Ubungo one, Tegeta, Nyakato Mwanza megawati
60, Ubungo two ya gesi na kampuni ya Symbion pamoja na IPTL na AGRECO
zinazotumia mafuta, ingawa serikali inaendelea kuongeza kiasi cha umeme huo kwa
kuwekeza katika gesi na makaa ya mawe.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment