Mzee Aboubakar Galiatano amezikwa kijiji Buganguzi katika halmashauri ya
Muleba mkoani Kagera akiwa na umri wa miaka 88, ameacha wajane 3 na
watoto 18, ilhali akiwa ni miongoni mwa wazee waliokuwa na historia
kubwa katika manispaa ya Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla, hasa
anapotajwa kupinga ubaguzi wa kidini, kuunganisha jamii na kuchochea
elimu pamoja na uwekezaji kibiashara.
Akizungumza katika ibaada ya maziko, shekh wa mkoa Haruna Kichwabuta amesema kuwa jambo la msingi kwa mwanadamu ni kuacha alama itakayokumbukwa hasa kukumbukwa kwa mema kama mzee Galiatano.
Na Mwanaharakati.
No comments:
Post a Comment