Jeshi
la Polisi mkoa wa Mwanza limeanza kuvunja mtandao wa majambazi wanaofanya
matukio ya uhalifu nchini, yakiwemo mauaji yanayoendelea wilayani Kibiti
mkoani Pwani, baada ya kuua majambazi sita kati ya wanane kwenye majibizano
makali ya risasi na majambazi hao.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, majambazi wawili kati
ya hao walifanikiwa kukimbia, hukuJeshi hilo likifanikiwa kukamata silaha za
kivita, mavazi ya kijeshi, bunduki za kienyeji, magazine, risasi pamoja na
nyenzo mbalimbali za kufanyia uhalifu.
Katika
majibizano hayo ya alfajiri yaliyodumu takribani saa mbili, katika eneo la
Fumagila kata ya Kishili wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, majambazi hao
walikuwa wamejificha ndani ya nyumba ndongo ya udongo, wakipanga mikakati ya
kufanya uhalifu.
Wakiwa
kwenye mjadala huo ghafla jeshi hilo liliizingira nyumba hiyo, na walipogundua
kuwa wapo chini ya ulinzi, kila jambazi akabeba silaha nzito kama njia ya
kujihami, ingawa jitihada zao hazikuzaa matunda kwa kuwa walishawaiwa, ingawa
majambazi wawili walikimbia.
Majambazi
wawili kati ya sita waliouwawa waligundulika kuwa ni wanachama wa mtandao wa
uhalifu wilayani Kibiti mkoani Pwani, akiwemo mkazi wa kata ya Kishili ambaye
hivi karibuni, aliwakimbia askari wa Jeshi hilo akiwa nyumbani na nyumba yake
kuchomwa moto na Wananchi wenye hasira.
Eneo
la Fumagila wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, ambalo limezungukwa na mapango ya
mawe limekuwa likitumika kama maficho ya majambazi, ambapo miezi kadhaa
iliyopita Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuuwa majambazi wengine kwa majibizano
ya risasi wakiwa Pangoni.
No comments:
Post a Comment