Mwalimu nyerere akiwa miongoni mwa kuhutubia wananchi,itakumbukwa kwamba
Ni
mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na
kutawala kwa miaka zaidi ya 24.Hapa ndipo mwili wake ulipohifadhiwa nyumbani kwake Butiama.
Mwishoni mwa maisha yake Nyerere aliishi kama mkulima wa
kawaida kijijini kwake Butiama. Alipatwa na kansa ya damu (leukemia) na
kufariki Uingereza wakati wa kutibiwa katika mji wa London tarehe 14
Oktoba, 1999. Alizikwa mahali pa kuzaliwa kwake, kijiji cha Butiama.
No comments:
Post a Comment