MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Tuesday 29 November 2011

Maadhimisho miaka 50 ya uhuru mkoani kagera yapambwa na wanafunzi. Maonesho hayo yalianzia maandamano katika kata ya rwamishenye yakiongozwa na wanafunzi wenyewe ambapo kufikia kona ya kyakairabwa darajani walikutana na trafik (askari wa usalama barabarani) wakaanza kuwapanga ni jinsi gani wataingia uwanjani kyakairabwa.

Mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa kagera katika maadhimisho hayo lakini kwa hakika yalihudhuliwa na wanafunzi kwa wingi ambapo watu wazima wachache sana waliojitokeza walizungumza nami wakadai hawana maslahi na hawaoni cha kuwakusanya kutokana na kwamba serikali madarakani ndiyo inafaida ma maadhimisho si wananchi hivyo hakuna haja ya kuudhulia.

Meya wa manispaa ya Bukoba Bwana ANATOL AMAN alihijiwa nami moja kwamoja akakiri uchache wa wa raia hao lakini akatoa sababu kuwa wamekosekana kwasababu ni siku za kazi na kutokana na uchumi wananchoi wapo kwenye shughuli za utafutaji.

Wanafunzi wenyewe walisema wamelazimishwa na walimu na katika shule ya Buhembe Sec School waliandakwa majina ambaye hakufika atapewa adhabu.


No comments: