NI mwalimu mkuu wa shule ya Kangabusharo Bw. PILIUS EMMANUEL akiwa ofisini kwake shuleni hapo. Analalamikia kuwa na walimu wa kiume pekee katika shule hiyo ambapo wanashindwa kulifundisha darasa la saba kwasababu wanafunzi wa kike katika darasa hilo wengi wanabalehe hivyo kulifanya darasa hilo kuwa katika hali mbaya ya hewa na uchafu kwani wengi wanaingia katika siku zao EDHI bila kujijua hivyo kuwafanya walimu kuona aibu katika darasa hilo.
Hawa ni wanafunzi katika darasa la tano wanaonekana wadogowadogo lakini baadhi ya mabinti nao wakianza kubalehe inakuwa ni chnagamoto kwa walimu hao wakiume waliopo shuleni hapo.
Mwalimu PILIUS alipohojiwa nami amesema ameshapeleka maombi katika ofisi ya afisa elimu wa wilaya ya Bukoba kupatiwa walimu wa kike ila anashangaa kuona kimya.
No comments:
Post a Comment