MASHIRIKA YANAYOSHUGHULIKA NA WAZEE KARAGWE (SAWAKA) NA KWA
WAZEE MULEBA.
Yamefanya semina ya siku moja na waandishi habari mkoani
Kagera kuona jinsi ya kushirikiana kufichua matatizo na kupata jinsi ya
kukabiliana nayo kupitia vyombo vya Habari mkoani humo.
Huyu ni Bi TEREZA EDWARD MINJA Mwenyekiti wa Tanzania Social
Protection Netwaork akitoa tamko la wazee, katika semina hiyo amesema bado
wazee wanalaumu serikali kutoweka sera ya wazee kisheria jambo linalosababisha
matamko ya serikali kwa wazee hao kutotekelezwa kama matibabu bure na pensheni.
Mzee maarufu mkoani kagera na Tanzania ambaye ni mwenyekiti
wa bodi ya kahawa Tanzania PIUS NGEZE amesisitiza kuwa serikali ijitahidi
kuwajali wazee kwani wanapofika umri wa uzeeni afya zao zinakuwa na matatizo
hivyo wasionekane bora wakiwa vijana uzeeni wakatengwa.
Hawa ni waandishi Habari mabo kwa upande wao wamesisitiza
ushirikiano wa mashirika ya saidia wazee Karagwe na Muleba kutoa ushirikiano na
wanapokuta tatatizo sehemu wawe tayari kuwajulisha waandishi ili wayatangaze
lakini kubwa zaidi washirikiane kuwezeshana kufika maeneo korofi.
No comments:
Post a Comment