Picha juu ni wachezaji wa Kagera Sugar wakitoka uwanjani kwa masikitiko baada ya kutoka sare na wachezaji wa African Lyon ambao nao hapa chini wanaonekana kusikitika sare hiyo.
Baada ya mchezo huo mmiliki wa African Lyon amelaumu waamuzi na kudai kuwa huo ni ubabaishaji huku akishindwa kutanabaisha tatizo analolalamikia lakini amedai TFF ina fanya upuuzi kwa kuwatumia waamuzi wasiyo na viwango.
Ndani ya mchezo huo mwamuzi ametoa kadi 3 za njano na nyekundu 1 kwa wachezaji wa African Lyon.
Uwanjani Kaitaba jumatato wiki ijayo kutakuwa na mtanange mwingine kati ya Kagera suga na Yanga Afrika.
No comments:
Post a Comment