Hawa ni Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo ambalo hata hivyo halikupata mwamko kutoka kwa wanakagera.
Jana jumamosi likafunguliwa kongamano la siku tatu katika manispaa ya Bukoba, ambalo hata hivyo linaendelea.
Lakini wakti huo Wananchi wamehimizwa kuienzi na kuitumia lugha ya Kiswahili, katika kukuza mawasiliano baina yao na watu wengine.
Aidha, vyombo vya habari, vinao wajibu wa kukuza na kuistawisha lugha ya
Kiswahili, kwa kuwa vinayo nafasi ya pekee ya kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi.
Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa KAGERA, bwana NASSOR MNAMBILA, alipomwakilisha mkuu wa mkoa, katika hotuba hiyo mkuu huyo wa mkoa amesema lugha ya Kiswahili ni mhimili muhimu katika kukuza mshikamano wa kitaifa.
Amesema takriba Watu Milioni 259 duniani wanaitumia lugha ya Kiswahili, hivyo kuna umuhimu wa kuiendeleza lugha hiyo.
Aidha, ameipongeza Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili-TATAKI, kwa jitihada zake katika kuikuza na kuistawisha lugha ya Kiswahili.
Profesa MUGYABUSO MULOKOZI, kutoka Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili, amesema kutumika kwa lugha ya Kiswahili katika mchakato wa kupata Katiba mpya ni kiashiria kizuri, kwa kuwa wananchi wengi watapata fursa ya kushiriki katika kuchangia mawazo yao.
Amewataka Watanzania kwa ujumla wao, waendelee kushinikiza na kudai Kiswahili kitambuliwe kuwa lugha rasmi ya kufundishia, na Kiingereza kisaidie.
Aidha, ameitaka serikali itunge Sera inayokitambua Kiswahili.
No comments:
Post a Comment