Rais Jakaya Mrisho kikwete amewasili Brazil
jana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika ziara
hiyo Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake
Rais Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais mstasafu wa nchi hiyo
Mheshimiwa Inacio Lula da Silva na viongozi waandamizi wa nchi hiyo.
Rais Kikwete
anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, mara tu baada ya hotuba
ya ufunguzi itakayotolewa na Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma
Rousseff wa Brazil, ambapo ataelezea maendeleo iliyofikia katika kuandaa mpango
kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi kama
ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete
anatarajiwa kurejea nchini Aprili 20, 2012.
No comments:
Post a Comment