THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho
kikwete anatarajia kuondoka leo tarehe 14 April, 2012, jioni kuelekea Brazil kwa
ajili ya ziara ya kikazi ya siku tano.
Katika ziara hiyo
Rais Kikwete anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais
Dilma Varna Rousseff wa Brazil na Rais
mstasafu wa nchi hiyo Mheshimiwa Inacio da Silva Lula na viongozi waandamizi wa
nchi hiyo.
Katika ziara hiyo,
Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi zinazoshiriki katika
Mpango wa Ubia wa Uwazi Serikalini (Open Government Partnership-OGP)
utakaofanyika mjini Brasilia chini ya Uenyekiti wa Rais Rousseff na kuhudhuriwa
na wajumbe wapatao mia nne (400) kutoka serikalini, Asasi zisizo za kiserikali,
Sekta binafsi pamoja na Mashirika ya Kimataifa.
Ubia wa Uwazi Serikalini au kwa kifupi OGP, ni mpango uliozinduliwa Septemba 2011 mjini New York, Marekani kwa lengo la kuwapa wananchi nafasi
ya kushiriki katika kuamua mambo
yanayowahusu, kupitia vyama visivyo vya Kiserikali na vya Kijamii.
Ubia huu
unashirikisha kwa usawa wawakilishi wa serikali kwa upande mmoja na wawakilishi
wa Asasi zisizo za Kiserikali za Kijamii kwa upande mwingine. Nchi ya Brazil
kwa kushirikiana na Marekani imekuwa mstari wa mbele katika kusukuma ubia huu.
Rais Kikwete
anatarajiwa kuhutubia mkutano huo tarehe 17 Aprili, asubuhi mara tu baada ya
hotuba ya ufunguzi itakayotolewa na
Mwenyekiti wa mkutano huo Rais Dilma Rousseff ambapo ataelezea maendeleo
iliyofikia katika kuandaa mpango kazi wa kutekeleza ahadi ya kuongeza uwazi
kama ilivyokubaliwa katika kikao kilichofanyika Disemba 2011.
Rais Kikwete
anatarajiwa kurejea nchini tarehe 20 Aprili, 2012.
…………Mwisho……………
Imetolewa na Premi
Kibanga,
Mwandishi wa Habari
wa Rais, Msaidizi
Ikulu
Dar-Es-Salaam
14 April, 2012
No comments:
Post a Comment