TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
A.MSIBA
WA KANUMBA
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinaungana na wasanii wote
nchini na Watanzania kwa ujumla kuombeleza kifo cha msanii mahiri Steven
Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi jijini Dar es Salaam.
B.PONGEZI KWA SIMBA
KUINGIA 16 BORA
TASWA
inatoa pongezi za dhati kwa timu ya Simba ya Dar es Salaam baada ya kufanikiwa
kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika
(CAF) kwa kuitoa ES Setif ya Algeria Ijumaa iliyopita.
Tunawasihi wachezaji wa Simba
na viongozi pamoja na mashabiki wa klabu hiyo, wasibweteke na mafanikio hayo
badala yake waunganishe nguvu ili waingie hatua inayofuata hatimaye watwae
ubingwa maana hakuna lisilowezekana chini ya jua.
C. WAANDISHI WALIOSHINDA
TUZO
Kamati ya Utendaji ya
TASWA inatoa pongezi za dhati kwa waandishi wa habari za michezo walioshinda
Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) zilizofanyika hivi karibuni jijini
Dar es Salaam.
Waandishi hao ni Imani
Mani aliyeshinda upande wa magazeti, Anwar Mkama upande wa televisheni na
Abdallah Majura upande wa redio, ambao tunaamini juhudi za kazi zao
zimefanikisha kupata tuzo hizo.
Nawasilisha.
Amir
Mhando
Katibu
Mkuu TASWA
08/04/2012
No comments:
Post a Comment