UNITED
REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa
Shirikisho la Filamu Tanzania
–TAFF- kuomboleza kifo cha msanii maarufu nchini Steven Charles Kanumba,
aliyeaga dunia usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, Aprili 7, 2012.
Katika
salamu hizo, Rais Kikwete amemwomba kiongozi huyo wa TAFF kufikisha salamu za
rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wana-familia ya Kanumba na kwa wasaani
wote nchini ambao wamepotelewa na mdau na mwenzi wao.
Rais
Kikwete amesema kuwa ameshtushwa na kuzunishwa na kifo cha msanii huyo ambaye
amemwelezea kuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa ambaye katika uhai wa
maisha yake mafupi na akiwa bado kijana sana amechangia kwa kiwango kikubwa
maendeleo ya sanaa ya filamu nchini na kupitia sanaa hiyo kuitangaza Tanzania
kimataifa.
Amesema
Rais: ”Nimepokea kwa mshtuko na huzuni nyingi taarifa za kifo cha Ndugu Steven
Charles Kanumba. Kupitia filamu zake, ameburudisha na kuelimisha jamii yetu kwa
namna ambayo haiwezi kupimika. Alikuwa msanii mahiri na mwenye kipaji kikubwa
ambaye mchango wake mkubwa katika kuanzisha, kukuza na kuimarisha sanaa ya
filamu nchini hautasahaulika.”
Ameongeza
Rais Kikwete: “Ndugu Kanumba pia ametoa mchango mkubwa katika kuitangaza nchi yetu ya Tanzania mbele
ya mataifa mengine kupitia sanaa ya filamu na uwezo mkubwa wa kisanii. Tutaendelea
kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa nchi yetu.”
“Nakutumia
wewe Rais wa TAFF salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako kwa wasanii wote
wa filamu na sanaa nyingine kufuatia msiba huu mkubwa kwa fani yetu ya sanaa.
Aidha, naomba unifikishie salamu za dhati ya moyo wangu kwa wanafamilia wote.
Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa. Waambie naelewa machungu yao
katika kipindi hiki kigumu cha msiba,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Namwomba
Mwenyezi Mungu awape subira na nguvu za kuweza kuhimili kipindi hiki kigumu kwa
sababu yote mapenzi yake. Aidha, naungana na wana-familia na wasanii wote
nchini kuwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya
Marehemu Steven Charles Kanumba. Amen.”
Mwisho.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
07 Aprili, 2012
No comments:
Post a Comment