
Akiongea na muandishi wa habari wa kituo hiki kwa niaba ya
wanafuzi wengine kituoni hapo, mtoto AGNES
JACKOB amesema kuwa wanajifunza ushonaji, kilimo na uselemara lakini
wanakumbana na uhaba wa vitendea kazi kama cheleani, mashine za kulandia mbao
na majembe kutokana na utaalamau wanaoendelea kuupata.
Mwanafunzi huyo ameongeza kuwa wanafrahishwa na mafunzo
wanayoyapata na kuongeza kuwa wakitoka wazisaidia familia zao hata kwa kutoa
mafunzo wanayoyapata.
Hizi ni baadhi ya kazi za watoto hao wamazofanya kwenye mazoezi yao kama unavyoona meza hapa chini.
Chini ni shamba la mfano la kilimo cha viazi ambalo limeandaliwa na wanafunzi wenyewe.
Kituo cha kusaidia watoto yatima na wanafunzi kutoka kwenye familia duni cha SAIDIA YATIMA NA WATEGEMEZI MISENYI kilichopo kijijini MUSHASHA, kina jumla ya wanafunzi 42 wakiwemo wakiume 23 na wa kike 21 kutoka halmashauri mbalimbali mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment