MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 30 July 2012

GAZETI MWANA HALISI KUFUNGIWA


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

TAMKO LA SERIKALI

GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imelifungia kutochapishwa gazeti la MwanaHalisi kuanzia 30 Julai, 2012 kwa muda usiojulikana kutokana na mwenendo wake wa kuandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi likiwa na nia ya kusababisha wananchi kukosa imani na vyombo vya dola hali inayoweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.

Katika matoleo yake hivi karibuni, gazeti la MwanaHalisi toleo Na. 302 la Jumatano Julai, 11 – 18, 2012 na toleo Na. 303 la Jumatano Julai 18 – 24, 2012 na toleo Na. 304 la Jumatano Julai 25 hadi 01 Agosti, 2012 na mengine yaliyotangulia yamekuwa yakichapisha habari na makala zenye kueneza na kujenga hofu kwa jamii.

Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, ameitwa na kuonywa mara nyingi, lakini hataki kukiri kuwa maudhui ya makala zake hazina tija kwa jamii, pia hazifuati weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Mhariri, mara zote katika utetezi wake amekuwa akinukuu kifungu cha 18 cha Katiba ya nchi yetu ambacho kinatoa uhuru wa kutoa maoni na kwa makusudi kutonukuu kifungu cha 30 cha Katiba hiyo kinachoweka ukomo wa uhuru.

Uamuzi wa Serikali
Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i), adhabu hiyo itaanza tarehe 30 Julai, 2012 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali (Government Notice) Na. 258 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali na kutolewa jijini Dar Es Salaam tarehe 27 Julai, 2012.

Serikali inawataka wamiliki, wahariri na wanahabari kuzingatia sheria, uzalendo, weledi na maadili ya taaluma ya uandishi wa habari katika kutekeleza wajibu wa kuhabarisha, kuelimisha na kutoa burudani kwa wananchi.

Kama ilivyoelezwa Bungeni wakati wa kuwasilisha Bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo hivi karibuni waandishi na watangazaji wa habari wanatakiwa kuhakikisha kuwa habari wanazoziandika na vipindi wanavyoandaa vinazingatia taaluma na kuweka mbele maslahi ya Taifa letu na uzalendo. Uhuru na haki ya vyombo vya habari uendane na wajibu.
Kuanzia sasa Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya vyombo vya habari ambavyo kwa maksudi vitatoa taarifa za uchochezi ambazo zitahatarisha hali ya amani na utulivu uliopo nchini mwetu.

Imetolewa na

OFISI YA MSAJILI WA MAGAZETI
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
30 Julai, 2012

WAZIRI KAWAMBWA ATAADHARISHA WALIMU

 Katika mikoa yote tanzania hali imekuwa ngumu baada ya mgomo huo maswali yamekuwa mengi kutoka kwa wananfunzi nakutupa mashaka je wanafunzi hao hawajachochewa na walimu?

Kauli ya Dk Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa;
“Nawashauri walimu wasigome kwa sababu Serikali imekubali kuwaongezea asilimia 15 ya mshahara, lakini haina uwezo wa kuwapa nyongeza wanayoitaka ya asilimia 100,” alisema Dk Kawambwa.
Alisema anafahamu kwamba walimu wanastahili kiasi wanachokiomba lakini tatizo ni kwamba Serikali haina uwezo wa kuwalipa kiasi hicho.
“Hata madaktari, Serikali inafahamu kwamba wanastahili kulipwa fedha walizoomba, lakini tatizo limekuwa uwezo wa Serikali kuwa mdogo,” alisema Kawambwa.
Juzi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alikaririwa akisema walimu watakaogoma watahesabiwa kuwa watoro na watachukuliwa hatua za kinidhamu kwa sababu mgomo huo sio halali.
Madai ya walimu
Madai ambayo walimu wamekuwa wakitaka ni ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa sayansi ya asilimia 55, asilimia 50 walimu wa masomo ya sanaa na asilimia 30 kwa walimu wanaofundisha katika mazingira magumu.
Naye Geofrey Kahango anaripoti kutoka Mbeya kwamba CWT Mkoa wa Mbeya kimesema kinaunga mkono mgomo wa walimu unaoanza leo (Jumatatu).
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Mbeya, Nelusigwe Kajuni aliwataka walimu wote wa Mkoa wa Mbeya kuwaunga mkono wenzao nchi nzima kwa kutofika kazini.
“Mgomo wa walimu upo pale pale na unaanza kesho (leo) saa 1:00 asubuhi. Mgomo wetu ni wa kutofika kazini na hautakuwa na ukomo hadi Serikali itakapokubali kutekeleza madai yetu,” alisema Kajuni.
Alisema kuwa madai ya walimu ambayo Serikali imeshindwa kuyatekeleza ni pamoja na kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa asilimia 50 katika masomo ya sanaa na asilimia 55 kwa masomo ya sayansi.
Kajuni aliyataja madai mengine kuwa ni posho ya kufundishia katika mazingira magumu asilimia 30 ya mshahara wa mwalimu na kuboreshwa kwa mazingira ya kufundishia kwa walimu wote nchini.
Alisema baada ya Serikali kupuuza madai ya walimu, sasa wameamua kutumia haki yao ya kisheria ya kugoma hadi pele ambapo madai yao yatasikilizwa.
Alisema hadi sasa Serikali inafanya propaganda za kuwatisha walimu wasigome, lakini haijachukua hatua za kisheria kuzuia mgomo huo kwa kuwa hadi sasa hakuna zuio lolote la mgomo lililotolewa mahakamani.
Kajuni aliwataka walimu wote mkoani Mbeya kusikiliza maelekezo kutoka CWT na sio propaganda na vitisho vinavyotolewa na Serikali kwa kuwa mgomo huo umefuata taratibu zote za kisheria.
Kutoka Pwani,  Julieth Ngalabali anaripoti kuwa  chama hicho kimesema kimeunga mkono kwa asilimia mia moja utekelezaji mgomo wa walimu.
Alisema katika mkoa wa Pwani tayari maelekezo muhimu ya azimio hilo kwenye shule zote na baadhi yao walikutana mjini Kibaha kupata taarifa zaidi juu ya utekelezaji.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Pwani, John Kirumbi alisema: “Sisi mpaka Ijumaa Baraza la Taifa la Chama limekutana nasi na kuazimia kutoa saaa 48 kwa Serikali… Hivyo utekelezaji wa mgomo tunaanza Jumatatu (leo).”

Aliongeza:  “Tunajua wanafunzi wetu wataboreka lakini sisi kama walezi wao tunalazimika kufanya hivyo ili hata na wao baadae waweze kupata huduma bora zinazostahili kutoka kwa walimu wao.”

Alifafanua: “Hili linawezekana tu pale mlezi wao mkuu ambaye ni Serikali itakapojibu madai yetu. Hivyo tunaishauri Serikali kama kweli ina nia njema naTaifa hili basi iache uonevu kwa walezi wa watoto hao ambao ndio wao wanaoliandaa Taifa la baadae.”
Kutoka Tanga, Burhani Yakubanaripoti kuwa walimu  mkoani humo wameamriwa kuanza rasmi mgomo wao leo kama ulivyopangwa.
Msimamo huo ulitolewa jana kwa vyombo vya habari na uongozi wa CWT mkoa baada ya kufanya kikao makao makuu ya chama hicho mkoani hapa.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Tanga, Sufian Mussa aliwataka walimu katika shule zote kutomsikiliza kiongozi yeyote wa Serikali.
Alisema kuwa Serikali ilipaswa kukutana na walimu mapema kabla ya kuendeleza vuguvugu hilo baada ya kuona mgomo wa walimu unapamba moto.
“Mgomo huu ni halali kisheria walimu wasiwe na woga wowote na wasifuate wala kusikiliza kauli ya kiongozi yeyote wa serikali,” alisema Mwenyekiti huyo.
Katibu wa CWT Mkoa wa Tanga , Ndelamio Mangesho alisema madai ya walimu yamegawanyika katika makundi matatu; nyongeza ya asilimia 100 ya mishahara kwa walimu wanaoanza kazi, kurejeshwa kwa malipo ya posho ya kufundishia kwa asilimia 50 na asilimia 55 kwa wale walimu wa masomo ya sayansi.
“Madai mengine ni asilimia 30 ya posho ya mazingiramagumu ya walimu ili wawe na hamu na mwamko wa kufanya kazi katika mazingira magumu,” alisema Katibu huyo.


Sunday, 29 July 2012

TUME YA TAIFA TA TAKWIMU YAHITIMISHA MAFUNZO KWA WAANDISHI HABARI NCHINI, JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAAZI

Afisa uhamasishaji Sensa Makao makuu Bw. Said J. K. Ameir
Ni baada ya kushiriki waandishi wa vyombo binafsi na serikali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati ambapo wamejifunza maana ya sense, malengo, faida na jinsi ya kuhesabu ikiwemo kutambua maeneo ya sense.
Awali wakati wa ufunguzi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evalist Ndikilo, amesema kuwa sensa ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee kwa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwani itawezesha kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa malengo ya millennia.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo kwenye ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati, inayohusu sense ya watu na makaazi, akiwasisitiza kutumia kalamu zao kuwaambia watanzania kujitokeza na kutoa ushiriki wao katika zoezi hilo muhimu litakalofanyika kuanzia usiku wa Agost 26 mwaka huu.
Amesema kuwa ni muhimu kwani raslimali watu ndiyo muhimili wa taifa, hivyo hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa pasipokuwa na uhakika wa idadi ya wakaazi nchini.
Hata hivyo amesisitiza kuwa wananchi wasiwe na shaka wakati wa zoezi hilo, kwani halitaathili shughuli zozote za kijamii, bali kuboresha kwani lengo kuu la sense ni kusaidia kupatikana kwa mipango mizuri ya maendeleo.

Maana ya kufanya sensa nchini ni kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha au kusambaza takwimu za kijamii kuhusiana na watu wote nchini na makaazi yao kwa kipindi maalum.
Sensa kwa waandishi hao wa habari kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na mikoa ya kati imewashirikisha waandishi zaidi ya 150 kutoka vyombo binafsi na vya serikali.