Kauli ya Dk Kawambwa
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa;
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa;
“Nawashauri walimu wasigome kwa sababu Serikali imekubali
kuwaongezea asilimia 15 ya mshahara, lakini haina uwezo wa kuwapa nyongeza
wanayoitaka ya asilimia 100,” alisema Dk Kawambwa.
Alisema
anafahamu kwamba walimu wanastahili kiasi wanachokiomba lakini tatizo ni kwamba
Serikali haina uwezo wa kuwalipa kiasi hicho.
“Hata
madaktari, Serikali inafahamu kwamba wanastahili kulipwa fedha walizoomba,
lakini tatizo limekuwa uwezo wa Serikali kuwa mdogo,” alisema Kawambwa.
Juzi,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alikaririwa akisema
walimu watakaogoma watahesabiwa kuwa watoro na watachukuliwa hatua za kinidhamu
kwa sababu mgomo huo sio halali.
Madai ya walimu
Madai ambayo walimu wamekuwa wakitaka ni ongezeko la mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa walimu wa sayansi ya asilimia 55, asilimia 50 walimu wa masomo ya sanaa na asilimia 30 kwa walimu wanaofundisha katika mazingira magumu.

Naye
Geofrey Kahango anaripoti kutoka Mbeya kwamba CWT Mkoa wa Mbeya kimesema
kinaunga mkono mgomo wa walimu unaoanza leo (Jumatatu).
Mwenyekiti
wa CWT Mkoa wa Mbeya, Nelusigwe Kajuni aliwataka walimu wote wa Mkoa wa Mbeya
kuwaunga mkono wenzao nchi nzima kwa kutofika kazini.
“Mgomo
wa walimu upo pale pale na unaanza kesho (leo) saa 1:00 asubuhi. Mgomo wetu ni
wa kutofika kazini na hautakuwa na ukomo hadi Serikali itakapokubali kutekeleza
madai yetu,” alisema Kajuni.
Alisema
kuwa madai ya walimu ambayo Serikali imeshindwa kuyatekeleza ni pamoja na
kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100, posho ya kufundishia kwa
asilimia 50 katika masomo ya sanaa na asilimia 55 kwa masomo ya sayansi.
Kajuni
aliyataja madai mengine kuwa ni posho ya kufundishia katika mazingira magumu
asilimia 30 ya mshahara wa mwalimu na kuboreshwa kwa mazingira ya kufundishia
kwa walimu wote nchini.
Alisema
baada ya Serikali kupuuza madai ya walimu, sasa wameamua kutumia haki yao ya
kisheria ya kugoma hadi pele ambapo madai yao yatasikilizwa.
Alisema
hadi sasa Serikali inafanya propaganda za kuwatisha walimu wasigome, lakini
haijachukua hatua za kisheria kuzuia mgomo huo kwa kuwa hadi sasa hakuna zuio
lolote la mgomo lililotolewa mahakamani.
Kajuni
aliwataka walimu wote mkoani Mbeya kusikiliza maelekezo kutoka CWT na sio
propaganda na vitisho vinavyotolewa na Serikali kwa kuwa mgomo huo umefuata
taratibu zote za kisheria.
Kutoka
Pwani, Julieth Ngalabali anaripoti kuwa chama hicho kimesema kimeunga
mkono kwa asilimia mia moja utekelezaji mgomo wa walimu.
Alisema katika mkoa wa Pwani tayari maelekezo muhimu ya azimio hilo kwenye shule zote na baadhi yao walikutana mjini Kibaha kupata taarifa zaidi juu ya utekelezaji.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Pwani, John Kirumbi alisema: “Sisi mpaka Ijumaa Baraza la Taifa la Chama limekutana nasi na kuazimia kutoa saaa 48 kwa Serikali… Hivyo utekelezaji wa mgomo tunaanza Jumatatu (leo).”
Aliongeza: “Tunajua wanafunzi wetu wataboreka lakini sisi kama walezi wao tunalazimika kufanya hivyo ili hata na wao baadae waweze kupata huduma bora zinazostahili kutoka kwa walimu wao.”
Alifafanua: “Hili linawezekana tu pale mlezi wao mkuu ambaye ni Serikali itakapojibu madai yetu. Hivyo tunaishauri Serikali kama kweli ina nia njema naTaifa hili basi iache uonevu kwa walezi wa watoto hao ambao ndio wao wanaoliandaa Taifa la baadae.”

Tanga, Burhani Yakubanaripoti kuwa walimu mkoani humo wameamriwa kuanza
rasmi mgomo wao leo kama ulivyopangwa.
Msimamo huo ulitolewa jana kwa vyombo vya habari na uongozi wa CWT mkoa baada ya kufanya kikao makao makuu ya chama hicho mkoani hapa.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Tanga, Sufian Mussa aliwataka walimu katika shule zote kutomsikiliza kiongozi yeyote wa Serikali.

kuwa Serikali ilipaswa kukutana na walimu mapema kabla ya kuendeleza vuguvugu
hilo baada ya kuona mgomo wa walimu unapamba moto.
“Mgomo
huu ni halali kisheria walimu wasiwe na woga wowote na wasifuate wala
kusikiliza kauli ya kiongozi yeyote wa serikali,” alisema Mwenyekiti huyo.
Katibu
wa CWT Mkoa wa Tanga , Ndelamio Mangesho alisema madai ya walimu yamegawanyika
katika makundi matatu; nyongeza ya asilimia 100 ya mishahara kwa walimu
wanaoanza kazi, kurejeshwa kwa malipo ya posho ya kufundishia kwa asilimia 50
na asilimia 55 kwa wale walimu wa masomo ya sayansi.
“Madai
mengine ni asilimia 30 ya posho ya mazingiramagumu ya walimu ili wawe na hamu
na mwamko wa kufanya kazi katika mazingira magumu,” alisema Katibu huyo.
No comments:
Post a Comment