Afisa uhamasishaji Sensa Makao makuu Bw. Said J. K. Ameir
Ni baada ya kushiriki waandishi wa vyombo binafsi na
serikali kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati ambapo wamejifunza maana ya sense,
malengo, faida na jinsi ya kuhesabu ikiwemo kutambua maeneo ya sense.
Awali wakati wa ufunguzi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi
Evalist Ndikilo, amesema kuwa sensa ya mwaka huu ina umuhimu wa kipekee kwa
jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwani itawezesha kwa kiasi kikubwa utekelezaji
wa malengo ya millennia.
Mkuu huyo wa mkoa ametoa kauli hiyo kwenye ufunguzi wa
semina kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya kanda ya ziwa na kati, inayohusu
sense ya watu na makaazi, akiwasisitiza kutumia kalamu zao kuwaambia watanzania
kujitokeza na kutoa ushiriki wao katika zoezi hilo muhimu litakalofanyika
kuanzia usiku wa Agost 26 mwaka huu.
Amesema kuwa ni muhimu kwani raslimali watu ndiyo muhimili
wa taifa, hivyo hakuna maendeleo yanayoweza kufikiwa pasipokuwa na uhakika wa
idadi ya wakaazi nchini.
Hata hivyo amesisitiza kuwa wananchi wasiwe na shaka wakati
wa zoezi hilo, kwani halitaathili shughuli zozote za kijamii, bali kuboresha
kwani lengo kuu la sense ni kusaidia kupatikana kwa mipango mizuri ya
maendeleo.
Maana ya kufanya sensa nchini ni kukusanya, kuchambua,
kutathmini na kuchapisha au kusambaza takwimu za kijamii kuhusiana na watu wote
nchini na makaazi yao kwa kipindi maalum.
Sensa kwa waandishi hao wa habari kutoka mikoa ya kanda ya
ziwa na mikoa ya kati imewashirikisha waandishi zaidi ya 150 kutoka vyombo
binafsi na vya serikali.
No comments:
Post a Comment