Taarifa kutoka afisi ya rais
zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu
usiku.
Msaidizi wake pia amethibitisha
kufariki kwa kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili
duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena
urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri
mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y
kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo
alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa
afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana,
Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi
hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda
katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa
ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa
Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na
kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana
" taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills
mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi
yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye
hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya
Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae
kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha
uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
No comments:
Post a Comment