MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 13 September 2012

SERIKALI YA MKOA YAAGIZA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA WENYE ULEMAVU YA MWAKA 2010

 Katika kutekeleza sheria hiyo, serikali ya mkoa wa Kagera imeagiza idara zote na mamlaka mbalimbali kupanua na kuhimarisha fursa za kisiasa, kiuchumi na ajira kwa walemavu wa aina zote. Pili kuhimarisha na kuboresha mbinu za ulinzi madhubuti katika kuzuia mauaji ya kikatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.
 Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii mkoani Kagera Rebeca Gwambasa, ameitaka jamii kuondoa ubaguzi wa rangi na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, kwani nao ni binadamu kama wengine.

No comments: