Mke wa Rais wa Zanzibar Mama
Mwanamwema Shein, amewataka wananchi kushiirikiana na Jeshi la Polisi Visiwani
humo katika kuwafichua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu mwambao
wa pwani ya visiwa hivyo ukiwemo uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya.
Mama Mwanamwema, ametoa wito huo leo
mjini Zanzibar, wakati akizindua kituo kipya cha Polisi cha Fumba kilichojengwa
kwa nguvu za wananchi na Wawekezaji katika wilaya ya Magharibi Zanzibar.
Mke huyo wa Rais wa Zanzibar amesema
kuwa kujengwa kwa kituo hicho ni kazi moja lakini kazi ya kuwafichua wahalifu
ni kazi ya pili ambayo inawategemea sana wananchi ambao ndiyo wanaoishi pamoja
nao.
Amesema kituo hicho kitasaidia kwa
kiasi kikubwa katika kukomesha vitendo vya kihalifu vikiwemo vya magendo, wizi
wa mifugo, usafirishaji na usambazaji wa madawa hayo ya kulevya ambayo yamekuwa
yakiathiri afya za vijana wa visiwa hivi na Tanzania kwa ujumla.
Amemtaka kila mwananchi kuhakikisha
kuwa anamfichua na kumtolea taarifa Polisi mhalifu yeyote ili achukuliwe hatua
ikiwa ni pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo
wake.
"Ndugu Wananchi, ninamategemeo
makubwa kuwa kituo hiki cha Polisi kitasaidia sana katika kupambana na matukio
ya kihalifu". Alisema Mama Shein.
Alisema taarifa zilizopo ni kuwa
maeneo haya yanachangamoto ya uhalifu wa aina mbalimbali, Wafugaji hapo salama
na mifugo yao na wakulima nao hawapo salama na mazao yao.
Awali akimkaribisha Mke wa Rais,
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, alisema kuwa, kwa kiasi
kikubwa, ujenzi wa kituo hicho umechangiwa na baadhi ya wafanyabishara yakiwemo
Mabenki, Shirika la Umeme na wawekezaji wa kigeni.
Amesema Jeshi la Polisi limesaidia
kuweka mafundi wa ujenzi na kugharimia baadhi ya mahitaji muhimu kwa lengo la
kufanikisha ujenzi huo na kuwasogezea huduma za kipolisi wakazi wa eneo hilo
ambalo kwa muda mrefu lilikuwa halina kituo cha Polisi.
Nao baadhi ya wananchi wamepongeza
juhudi binafsi zilizochukuliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi
zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, katika kuwashawishi wawekezaji wa kigeni na
mabenki kuchangia ujenzi wa kituo hicho.
Miongoni mwa Makampuni yaliyochangia
katika ujenzi huo ni Benki ya Wananchi wa Zanzibar BPZ na Shirika la umeme
Zanzibar ZECO.
hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa
makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Seif Iddi pamoja na Mkuu wa Mkoa
wa Mjini Magharibi Bw. Abdallah Mwinyi na Makamaba wa Polisi wa mkoa wa Mjini
na makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar.
Shein,akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Kituo cha Polisi cha
Fumba Mkoa Mjini Magharibi leo,(kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi
Abdalla Mwinyi Khamis,na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali
Baadhi ya Maofisa mbali mbali wa Jeshi la
Polisi Zanzibar wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein,akizungumza na wananchi wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo
cha Polisi Fumba Mkoa wa Mjini Magharibi leo.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema
Shein,akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Biashara na Huduma za
Wateja,Mussa Ramadhan Haji,kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maji (ZAWA) ikiwa ni miongoni waliochagia katika ujenzi wa Kituo cha
Polisi cha Fumba Mkoa Mjini Magharibi,wakati wa hafla ya ufunguzi wa
kituo hicho leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
No comments:
Post a Comment