MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Monday, 15 October 2012

ABIRIA WAENDELEA KUIBIWA KIVUKONI KIGONGO-BUSISI MKOANI MWANZA.

Kama inavyooneshwa kwenye Kibao kilichopo ofisi ya kulipisha na kutoa lisiti inayomruhusu abiria kuingia eneo la Kivuko, baada ya kuingia ndani ya eneo hilo unakutana na sehemu iliyojengwa ikionesha kuwa abiria wote wanatakiwa kupumzika ndani ya banda hilo la serikali.

Kilichonifanya kufuatilia zaidi ni pale ambapo nimekuta abiria wanaopumzika kwenye banda hilo la serikali kulazimishwa kulipia shilingi miamoja za kitanzania ili kujisaidia ndani ya vyoo vilivyopo ndani ya jingo hilo kwa ajili ya abiria.
Swali langu hapa ni kwanini watu wazima walipie shilingi 400 wakati wa kuingia eneo hilo na pia watakiwe kulipia sh 100 ili wajisaidie?
Kibaya zaidi unapolipia wala hupewi lisiti ya kulipia hiyo shilingi mia, nilipo dadisi zaidi nilijibiwa lugha ambayo haikunifrahisha, lakini vijana wanaoonekana pichani ndiyo wanaolipisha na nilipowauliza alipo bosi wao walisema hawajui alipo wakati lakini wakanitajia jina moja tu la TOM, je ni haki kulipisha watu paspokutoa stakabadhi?



Nicolaus Mac Ngaiza, nikiwa ndani ya Kivuko cha eneo hili kiitwacho MV SENGEREMA.


No comments: