Tukio hilo ambalo limethibitishwa na
kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow linadaiwa kutokea majira ya
saa 4: 13 usiku wakati afisa huyo wa uhamiaji akiwa njiani kuelekea
nyumbani kwake ambapo alikutana na gari dogo aina ya Suzuki lililomuashia taa
likimuashiria kusimama.
Akielezea mkasa kamili Buchafwe
alisema kwamba baada ya kuwashiwa alipochunguza kwa makini gari hilo aliweza
kulibaini kuwa ni lile linalotumika na afisa huyo wa Polisi, hivyo alisimama na
kujitambulisha kwake akiwa ndani ya gari lakini aliamuriwa kuzima taa za gari
lake na kutoka ndani yake.
Alisema wakati bado akijitambulisha
alishuka askari aliyekuwa na sale katika gari hilo la afisa huyo wa polisi
akiwa na silaha ya SGM hali ambayo ilimlazimu kugeuza gari haraka na kukimbia
huku gari lake likishambuliwa nyuma kwa risasi.
“Gari langu limeshambuliwa kwa
risasi zaidi ya tano, moja imetoboa upande wa mbele karibu na Taili ya kulia,
risasi tatu zimetoboa nyuma ya gari na moja ubavuni mwa gari upande wa nyuma,
lakini sikuweza kupata madhara hali ambayo ilinilazimu kukimbia hadi ofisini
kwangu na kutoa taarifa kwa bosi wangu wa mkoa usiku huo,” alizidi kufafanua.
Buchafwe alisema amepatwa na mashaka
na tukio hilo kutokana na asakri huyo aliyehusika kuwa na mahusiano ya karibu
na mkewe ambaye wamekuwa na ugomvi naye pamoja na kesi ya kutalikiana
mahakamani na kusema kwamba huenda ahalikuwa la bahati mbaya.
“Nina kesi na mke wangu mahakamani,
na afisia huyu wa polisi amekuwa na mahusiano ya karibu na mke wangu huyu ambaye
tunashitakiana mahakamani, inanishangaza kwamba mtu ambaye ananifahamu licha ya
kujitambulisha bado alikuwa akishilikilia msimamo wa kunitaka kushuka, nadhani
hapa kuna jambo zaidi ya hali ilivyo,” alieleza.
Aidha akizungumzia tukio hilo
kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza alikiri kuwapo kwake na kudai kwamba anayo
hakika kwamba tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya kwani jeshi lake lilipata
taarifa za Kiinterejensia za kuwapo kwa majambazi wakidaiwa kutumia gari sawa
na ambalo afisa huyo wa uhamiaji alikuwa nalo.
“Hili ni tukio la bahati mbaya,
jeshi laetu lilipata taarifa za Kiinterejensia juu ya kuwapo kwa majambazi na
kuamua kuweka mtego, sasa afisa huyu alifika muda na wakati ambao askari wetu
walikuwa eneo hilo na kuingia katika mtego wetu, alikuja na gari ambalo ni sawa
na lile ambalo tulielezwa kuwa lingetumika, lakini bahati nzuri mauaji
hayakutokea,” alifafanua kamanda huyo.
Kamanda Barlow amedai kwamba
kutokana na tukio hilo amepanga kukutana na afisa huyo wa uhamiaji na
kuzungumza naye akiwa na askari wake kutafuta suluhu ya jambo hilo ambalo
aliekeza kwamba yeye anaamini limetokana na bahati mbaya.
No comments:
Post a Comment