Waziri wa serikali
, Asuman Kiyingi, alisema kuwa dhana kuwa Uganda inaunga mkono waasi wa M23
katika DRC wakati ikiwa mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani ni njama ya
kuidhalilisha na kuiharibia sifa nchi hiyo.
Aliongeza kuwa ,
ikiwa madai hayo hayataondolewa dhidi yake pamoja na juhudi za nchi hiyo kukosa
kutambulika, serikali itaondoa wapatanishi wake kwenye mazungumzo ya amani.
Amesema pia vikosi
vya nchi hiyo vilivyo nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika ya Kati, pia
vitaondolewa.
Vikosi hivyo
vinaungwa mkono na Umoja wa Mataifa hatika harakati zao dhidi ya waasi na wanamgambo.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment