MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 25 October 2012

UZIDUZI WA UPANDAJI MITI WAFANYIKA MANISPAA YA BUKOBA, ILHALI MATATIZO YA KUKWAMISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UKIENDELEA MKOANI KAGERA.

 Mkuu huyo wa mkoa alianzisha mpango wa KAGERA GREEN BELT MOVEMENT, ambao hasa unawahusisha vijana ili kuondoa uzembe kwa vijana kujihusisha na vijiwe vya kahawa.

 Wakati upandaji huo wa miti ukianza rasmi, wanaharakati wa mazingira tumebaini uwepo wa viashiria vya kuendeleza uharibifu wa mazingira kama picha yetu chini inavyoonesha mbao ambazo zinakatwa bila kufuata utaratibu wa kata mti panda mti.
 Kama hiyo haitoshi uchomaji wa mkaa nao waendelea kama inavyoonekana katika picha yetu hapa chini, lakini pia picha chini zaidi inaonesha wananchi wakikaa sehemu inayozuiliwa kukalia ili mazingira yabaki salama, je watu hao hawajui kusoma, au ni vipofu?

 Wakati huo huo bila kutenga maeneo mbadala kwa wachuuzi wadogowadogo, ni lazima miti inayopandwa itang'olewa ili machinga hao waendelee kuuza biashara zao kandokando ya barabara hizo mjini Bukoba.
 Kinachonishangaza zaidi, ni pale ambapo tunakazana kupanda miti ilhali barabara baadhi bado ni mbovu, je wakati wa ukarabati miti hiyo ukingoni mwa barabara haing'olewa kupisha upanuzi? Wakati mwingine wapo wachache wasiojua maana ya kujenga kando ya barabara wanaamua kuweka hata shule kama inavyoonekana hapo chini, ni maeneo ya kandokando ya ziwa.


 Ndugu zanguni haya tuyaite maisha magumu au? Ni kijana mmoja akiokota makopo ambayo yametupwa kwenye mto unaomwaga maji yake katika mto Kanoni Manispaa ya Bukoba, sasa je tunatunza mazingira?
 Nimejiuliza ni kwa vipi Bukoba wanaweza kuirekebisha manispaa ikawa kama unavyoona hii picha chini ambayo nimeichukua mkoani Singida.
 The man of tarlent nikiwa katika usafishaji wa mazingira ofisini kwangu Kasibante Redio.
MWANA HARAKATI

No comments: