MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 14 October 2012

USAFI WA MAZINGIRA KATIKA JIJI LA MWANZA UKOWAPI?

 Hapa ni katika eneo la Kirumba karibu na mtaa wa Mwaloni ambapo shughuli mbalimbali za raia zinaendelea lakini kubwa zaidi ni wafanyabiashara, na pamoja na hiyo kumeonekana maeneo mengi yana magofu au majengo ya zamani yasiyo na ubora mengine kama yanavyoonekana kubomoka na kutia madoa katika jiji hilo.
 Hii barabara iliyoko karibu na VLA PACK HOTEL ndani ya jiji hilo karibu kabisa na uwanja wa CCM KIRUMBA.
 Jengo hili chini lipo kwenye barabara pacha itokayo karibu na jengo la jiji ambapo hata chini yake panaonekana kukanda kwa mazingira.
 Kutokana na Taswira inayoonekana katika jiji hilo, Kamera yetu imebaini kuwa usafi huo upo katika maeneo yan ayofikiwa na wakubwa tu ikiwa ni pamoja na mahotel maarufu, uwanjwa wa ndege ofisi za jiji pamoja na sehemu za kati mwa jiji ambazo hata hivyo zimepakana na jiji tofauti na hapo maeneo mengine ni machafu.

 Picha juu ikiwa ni Hotel ya La Kairo, chini ni maeneo ya Airpot Mwanza ambapo usafi unaonekana kuhimarika kwa kiwango kikubwa.


 Hata hivyo kutokana na uwekezaji wa hapa na pale unaoendelea kuonekana katika jiji hilo, inawezekana wakafaulu katika usafi kwani hakuna atakayekubali kukaa kwenye usafi huku akiitaji kupata kipato kupitia uwekezaji wake.
Hayo ni baadhi tu ya maeneo niliyoamua kutembelea ili kupata picha kuhusu jiji la Mwanza na usafi wa mazingira.

No comments: