Na
Adrophina Ndyeikiza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa DSM 19/10/2012
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amekutana na waandishi wa habari leo asubuhi katika Ofisi yake na kutoa tamko kuhusu vurugu zinazoendelea kujitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki amekutana na waandishi wa habari leo asubuhi katika Ofisi yake na kutoa tamko kuhusu vurugu zinazoendelea kujitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhe.Mkuu
wa Mkoa amesema kuwa kumeibuka vitisho vya hapa na pale katika Mkoa wa Dar es
Salaam baada ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda ambaye anajulikana kama Katibu
wa Baraza kuu na Taasisi za Jumuiya ya Kiislamu. “Mpaka sasa wametoa taarifa
kuwa kutakuwepo na maandamano ya kuelekea Ikulu ili kushinikiza kuachiwa huru
kwa Sheikh Issa Ponda na wafuasi wake”.
Alisema
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Maandamano hayo hayana kibali chochote kile ni
kutaka kuibua vurugu na uvunjifu wa amani kwa wana Dar es Salaam,hivyo basi
nawaomba wananchi wa Dar es Salaam kutokushiriki katika maandamano hayo kwani
kwa kufanya hivyo sheria kali zitachukuliwa dhidi ya waandamanaji kwani
maandamano hayo ni Haramu na hayana kibali wala tija kwa Taifa letu.
Alisisitiza
Mkuu wa Mkoa. Aidha,Mkuu wa Mkoa alisema kuwa lazima tufike mahali tuishi kwa
kufuata misingi ya taratibu na sheria za taifa letu kwani Sheikh Ponda
hakukamatwa kama Sheikh bali kama mchochezi wa vurugu na kuwashawishi wafuasi
wake kuidharau Serikali na vyombo vya usalama.Hivyo amekamatwa kama mtuhumiwa
mwingine yoyote anayeweza kukamatwa. Hivyo basi yatupasa
tuwe na subira na kufuata taratibu husika kwani kama Sheikh Issa Ponda hana
hatia basi ataachiwa na kama ana hatia basi atahukumiwa kama ilivyo kawaida kwa
mtuhumiwa yoyote yule akipatikana na hatia.
Hivyo basi lazima tujue kuwa nchi yetu inaongozwa
kwa misingi ya taratibu na sheria na hakua aliye juu ya sheria.Sheria ipo na
lazima ifuatwe. Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema Mihadhara
yote ya kidini kwa sasa imesimamishwa kwa kipindi hiki kigumu mpaka hapo hali
itakapokuwa shwari.
NAYE SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM- Sheikh Alhadi
Mussa amewataka waumini wa dini ya kiislamu kuwa na subira katika kulitatua
suala hili na wasijipange kufanya vurugu ya aina yoyote kwani suala hilo
limeshafika katika vyombo vya sheria hivyo tuviachie vyombo hivyo vifanye kazi
yake na haki itakuja kujulikana. Aidha Sheikh huyo amesema kuwa ameridhishwa na
maneno ya maaskofu katika kuwataka waumini wao kuwa na utulivu na si kulipiza
kisasi kwani.Lakini pia amewataka waislamu nao watulie katika hilo.
PADRI ANTHONY MAKUNDE –Katibu Mkuu wa Balaza la
Maaskofu(Tech) amesema kuwa anaungana na viongozi wengine wa makanisa katika
kuwasisitiza viongozi wa Dini ya Kikristo kuendelea kuwa na subira katika
kipindi hiki kwani njia pekee na sahihi ya kutafuta suluhu na amani ni njia ya
mazungumzo.
KWA UPANDE WA KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA DAR ES
SALAAM- Suleimani Kova amesema kuwa Jeshi la Polisi limeungana na Mhe.Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam katika kukabiliana na vurugu zitakazojitokeza katika Mkoa
wa Dar es Salaam.
Hata hivyo mtu yeyote akifanya kosa anachukuliwa
kama mharifu kwa sababu sheria haibagui wala kuchagua yenyewe inakata kotekote
haiangalii kama ni Padri au Sheikh. Kuhusu maandamano hayo yaliyopangwa Kamanda
kova amesema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vema katika kukabiliana na hilo
hivyo mtu yeyote akitaka kuandamana ajitahidi kutafakari mara mbili mbili
itakuwaje baada ya hapo kwa yeye na familia yake.
Kova amewataka watu hawa wajisalimishe wenyewe kwa
jeshi la polisi ama sivyo sheria itachukua mkondo wake. -Mukadam Salehe -Kondo
Juma -Saaban Mapeo -Jaffary Mneke -Rajabu Katimba -Amani Moshi
No comments:
Post a Comment