Kiongozi mmoja mkuu wa kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni
mbunge mteule ameshtakiwa kwa kuchochea ghasia.
Mbunge Sheikh Mohammad Dor alisema
kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la
Pwani.
Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh
Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo
Omar Mwamnuadzi.
Sheikh Dor alikamatwa jana jioni
baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa
aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka
ya uchochezi.
No comments:
Post a Comment