Balozi wa Ubalozi wa Kudumu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi amesema
hayo wakati Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na lililofunguliwa na
Katibu Mkuu Ban Ki Moon.
Mjadala huo ulihusu uhusiano kati ya
Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Miongoni mwa
mambo aliyosisitiza Balozi Manongi ni pamoja na kuishauri ICC kutenda haki bila
kuegemea upande wowote na kwamba ijitahidi kujiepusha na ushawishi wa kisiasa
kutoka nchi yoyote ile likiwamo Baraza Kuu la Usalama.
Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa
katika mkutano wake wa wazi uliokuwa ukijadili uhusiano kati ya Amani na
Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Na Maura Mwingira
No comments:
Post a Comment