MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 7 October 2012

WAZIRI MKUU PINDA AUDHURIA MISA YA KUTABARUKU KANISA KUU JIMBO LA BUKOBA LA MATER MISERICOBDIAE(MARIA MTAKATIFU MAMA WA HURUMA) PAMOJA NA KUWEKA SHADA LA MAUA KWENYE KABURI LA CARDINAL LAURIAN RUGAMBWA ALIYEZIKWA RASMI JANA KANISANI HUMO.


Katika misa hiyo, yamezikwa masalia ya watakatifu Mathias Mulumba na Kalori Ruhanga katika Altare ya kanisa hilo.

 Ikawa ndiyo fursa ya waziri mkuu kuweka shada la maua kwenye kaburi hilo, ambalo liko katikati ya makaburi mawili ya wazi ambapo moja limeandaliwa kuzikwa askofu wa sasa atakapofariki na lingine litasubiri askofu mwingine kwa mujibu wa Rais wa Baraza la maaskofu Tanzania TEC Askofu ALMACHIUS NGALALEKUMTWA ambaye hata hivyo ni Askofu wa jimbo kuu la Iringa alipomweleza Mhashama Askofu Nestorius Timanywa kuwa hiyo itakuwa nafasi yake atakapoitwa na Mwenyezi Mungu.

 Maaskofu wakikomnika kwa ajili ya kuwakomnisha maPadre na hatimaye nao kukomnisha waumini wengine.
 Barza la maaskofu katika kumuhenzi Rugambwa, wameamua kuwa chuo kikuu cha Mt Augustino tawi la Bukoba, kiitwe chuo kikuu LAURIAN RUGAMBWA.
Katika misa hiyo, Balozi wa Papa hapa nchini Askofu Conchesco, amesoma ujumbe wa Papa Benedicto wa 16, ukiwata wakatoliki kuwa wamoja huku akisisitiza kuwa jimbo la Bukoba lililojengwa na Mhadhama Rugambwa, litaendelea kuwa nguzo imara katika Tanzania kwani ndiye aliyekuwa askofu wa kwanza wa Tanzania, lakini pia Cardinal wa kwanza wa Afrika.

No comments: