MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Thursday, 27 December 2012

KOMBE LA MBUNGE LIKO PALEPALE.

 Amesema kuwa ni mipango ya wasimamizi wa soka Bukoba, kujiweka sawa kuhakikisha wanaondoa tofauti zao na wampe majibu ya kujipanga kwao ili waendelee, lakini akasisitiza kuwa lengo la kombe hilo ni kuinua vipaji vya vijana wa Bukoba wala si kama walivyokuwa wakifanya kuajiri wachezaji kutoka nje ya mkoa na hata nje ya nchi.

Amekiona kitendo hicho kama jambo la biashara na kushindwa kunufaisha wana Jimbo, hivyo amesema amesubiri wampe taarifa za kujipanga kwao ili 2013 kombe liendelee.
Hata hivyo waziri Kagasheki, amesema kuwa katika kipindi cha miezi7 ya uwaziri, alikuwa bado anapunguza changamoto alizokutana nazo pindi ameingia wizarani hapo, hivyo michakato inaendelea kuhakikisha hifadhi za mkoa wa Kagera zinakuwa za taifa ili kusaidia upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa mkoa huo.

No comments: