Mkuu wa wilaya ya BUKOBA,
bi ZIPPORAH PANGANI, amewatahadharisha
Wananchi mkoani KAGERA, kutojichukulia
sheria mkononi, pale wanapowatuhumu watu
kwa makosa mbalimbali.
Bi PANGANi, ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, ameonya kuwa hakuna mtu yeyote aliye
juu ya sheria, na kuwa yeyote
atakayevunja sheria, atashughulikiwa kwa
mujibu wa sheria.
Mkuu huyo wa wilaya ametoa
tahadhari hiyo baada ya kutembelea eneo la Majengo Mapya, Kata KASHAI, ambapo kundi kubwa la wananchi walikuwa
wamekusanyika.
Mtuhumiwa huyo, ambaye ni
mwanamke, amelazimika kupelekwa polisi,
baada ya watu wenye hasira kuingia ndani
ya nyumba yake, kufuatia kuwepo uvumi kuwa alikuwa anawahifadhi watoto sita, kwa
lengo la kuwafanyia vitendo vinavyodaiwa kuwa ni vya ushirikina.
Polisi wakipiga mabomu ya machozi ili kutawanya mamia ya raia waliotaka kuvunjwa nyumba ya mtuhumiwa huyo.Wanamgambo na askari polisi wakikusanya baadhi ya raia wanaosadikiwa kusha mawe katika vurugu hizo
Katika vurugu hizo, raia mmoja ambaye picha yake haikuwekwa hapa, ameripukiwa na bomu hilo na kumsababishia maumivu makali usoni na mikononi kupasuliwa vidole.
No comments:
Post a Comment