MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Wednesday, 19 December 2012

ZIMAMOTO YASHINDWA KUFIKA KWENYE TUKIO LA MOTO

Hii ni kutokana na miundombinu mibovu baada ya wananchi kujenga kwenye mlima mjini Bukoba, ambako hakufikiki na chombo chochote cha usafiri jambo ambalo limewafanya kikosi cha zimamoto kushindwa kufika kwenye nyumba moja iliyokuwa ikiwaka moto.
 Ni katika eneo la Kashura, na baada ya kuzungumza na askari wa zimamoto waliokuwa kwenye msafara, wamesema kuwa hii hali wanakumbana nayo mara kwa mara katika makaazi tofauti ya mji wa Bukoba, kutokana na ujenzi holela ambao hauzingatii sheria na taratibu za nchi.
 Picha chini ni njia itumiwayo na wakaazi wa eneo hilo ambapo katika tukio hilo tanesco walifanikiwa kufika na kuzima umeme pamoja na baadhi ya maeneo ambayo tayari yalikuwa yameshika moto, na hakuna aliyejuruhiwa wala kupoteza maisha.
MWANA HARAKATI

No comments: