MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 3 March 2013

NAPE: SERIKALI IUNDE TUME KUCHUNGUZA TUHUMA DHIDI YA MEYA MANISPAA YA BUKOBA

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mkoani Kagera, katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM NAPE NNAUYE, amesema kuwa tuhuma zinazomkabili meya ANATORY AMAN zinapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kina na zikibainika ni za kweli hatua kali zitachukuliwa.
 Amesema kuwa chama cha mapinduzi kinasikitishwa na tuhuma hizo kwani zinachafua chama na kuleta migogoro ya kushindwa kutekelezeka kwa ilani ya chama hicho, hivyo serikali ifanye haraka iwezekanavyo ili na chama kichukue atua zake.
 Kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa Bi BUHIYE, na Chini kushoto ni mkuu wa wilaya Bukoba Bi ZIPORAH PANGANI.
 Huyu hapa chini ndiye Meya Manispaa ya Bukoba Anatory Amani anayetuhumiwa kufanya mikataba isiyo sahihi kuhusu viwanja na soko la Bukoba.
MWANA HARAKATI

No comments: