MBUNGE wa jimbo
la Arusha mjini Godbles Lema ameachiwa kwa dhamana hadi tarehe 29 mwezi wa tano
kesi hiyo itakapotajwa tena katika Mahakamana hiyo.
Baada ya Mbunge
huyo kuachiliwa huru, umati wa wanachama wa Chadema waliokuwa wamejazana katika
Mahakama hiyo walifanya maandamano makubwa kwenda katika Ofisi za Chama hicho
zilizopo maeneo ya Ngarenaro.
Mbunge huyo
amekutwa na makosa matatu ambapo kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo
cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘.Haki
hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa
kupiganiwa.
Kosa la pili ni
pale alipotamka kuwa “Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na
mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye
send-off.
Kosa la tatu ni
pale alipotamka kwa wanafunzi kuwa “Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi
mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa Mkuu wa Mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na
haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa
mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa
kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment