Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu FABIAN MASSAWE,
ameshauri vyombo vya habari na Wana habari kuhamasisha jamii mkoani humo
kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Maadhimisho
ya Siku ya Mashujaa.
Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa hufanyika
kila tarehe 25 mwezi Julai. Kitaifa mwaka huu yatafanyika Julai 25, mkoani KAGERA, katika
kambi ya Jeshi la Wananchi-JWTZ-KABOYA, wilayani MULEBA.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk JAKAYA KIKWETE.
Kanali MASSAWE amesema
vyombo vya habari na Wanahabari
ni kiungo muhimu katika kuhamasisha jamii iweze kushiriki kikamilifu
katika maadhimisho hayo.
Ameshauri Wazee walioshiriki matukio wakati ule kujitokeza na kusimulia ili liwe fundisho kwa jamii ya sasa itambue uzalemdo wa kuipigania
nchi yao .
Aidha, amewataka Wakazi wa mkoa wa KAGERA kutumia
fursa hiyo kuwekeza zaidi na kupata ajira.
Picha juu na nichi ni baadhi ya waandishi habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia katika mkutano huo uliowashirikisha wadau wa habari pia.MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment