Wesley
Korir, aliyemaliza wa tano mwaka huu, amezungumzia hofu yake pindi aliposikia
milipuko miwili iliyotokea Boston

Milipuko hiyo ilitokea karibu na
msitari wa mwisho wa kumalizia mbio hizo na kuwajeruhi takriban watu 140
takriban saa mbili baada ya mshindi kumaliza mbio hizo.
''Ikiwa shambulio hilo lingetokea
saa mbili kabla ya mbio kumalizika labda ningekuwa miongoni mwa
waliojeruhiwa,'' alisema bwana Korir.
Alikuwa akisherehekea ushindi wa
mkenya Rita Jeptoo katika mbio za wanawake.
"furaha yetu ni kuwa tulikuwa
tayari tumeondoka katika eneo hilo,'' Korir aliambia BBC.
Bi Jeptoo anatoka katika eneo bunge
la Cherangany, ambalo bwana Korir ni mbunge wake baada ya kushinda katika
uchaguzi uliofanyika mwezi jana.
Licha ya milipuko hiyo pamoja na
jukumu lake la kisiasa, Korir amesema kuwa ataendelea kushindana katika mbio za
marathon hata ikiwa Boston itaandaa mbio zengine mwaka ujao.
Korir alisema kuwa aliogopa sana aliposikia kuhusu habari ya milipuko.Alisema kuwa punde tu baada ya kusikia habari hiyo aliwapigia simu wakwe zake kuwajulia hali kwani walikuwa wamemtembelea pamoja na kocha wake.
Balozi wa Kenya nchini Marekani amesema kuwa hana taarifa zozote kuhusu wakenya waliojeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.
Raia wawili wa Afrika Kusini walitibiwa baada ya kupata majeraha
Lelisa Desisa, wa Ethiopia alishinda mbio za wanaume mbele ya mshindani wake Micah Kogo.
Mbio hizo mwaka huu zilikuwa na wanariadha 23,000 na zilitazamwa na mamia ya mashabiki.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment