Wananchi wilayani Kyerwa mkoani Kagera, wamesema kuwa
wamesubiri utekelezaji wa viongozi kuwa tayari wameshajitenga kutoka Karagwe,
hivyo viongozi waliopangiwa huko watekeleze kazi zao kwakufuata maadili na
sheria za nchi.
Wamesisitiza kuwa bado wanakabiliwa na suala la miundombinu,
ambayo hatahivyo ni pamoja na barabara, zahanati, umeme na maji, ambavyo bila
kupatikana kwake haitaweza kuendelea kama
halmashauri zingine.
Katika upande mwingine, wapo wananchi wanaomlalamikia mbunge
wa jimbo hilo kuwa tangu ameingia madarakani
hajawai kutembelea eneo hilo hadi alipofika
rais, na pia amejenga shule kwenye eneo alilopenda yeye, wakinukuu kama hakuwalenga wananchi bali ni kwa maslahi binafsi.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment