Kutokana na hali ambayo wanafunzi wa shule hiyo wameilalamikia kwa zaidi ya miaka 5, mbunge jimbo la Bukoba mjini Balozi HAMIS KAGASHEKI, alipotembelea shule hiyo mwezi April mwaka huu, akaahidi kugharamikia ukarabati wa tank la maji ambalo hatahivyo awali aligharamikia ujenzi wake, lakini likajengwa chini ya kiwango na baadaye kushindwa kutumika kwani maji yalikuwa yakivuja.
Kiasi cha sh milioni 3, amekitoa na sasa ukarabati wa tanki umefanyika kwa gahara ya sh mil2.9 ambapo sasa huduma ya maji imeanza kupatikana kwani tayari tank hilo limekamilika ukarabati wake.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Mugeza akawaomba wazazi, walezi na wadau wa elimu kuendelea kuunga mkono juhudi za kusaidia katika masuala ya elimu.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment