Juu ni mtendaji kata Kashai, ambapo kumejitokeza miundombinu mibovu ya barabara, kufanyika miadhala na burudani katika maeneo ya shule wakati wa masomo, na uwingi wa wanafunzi wakati shule ni chache.
Juu na chini katika shule ya sekondari Buhembe, ambapo mdahalo umefanyika na kuibua wanafunzi kupungua kila mwaka kuanzia 2007 ilipokuwa na wanafunzi 351 na sasa 227 kutokana na kuhamishwa kwa viongozi mara kwa mara, ambapo kila uongozi unaleta taratibu zake ikiwamo kubadili sare za shule kila anapoingia mpya, jambo lingine wazazi kutochangia gharama za masomo za mwanafunzi.
Chini ni kata Kitendaguro, wao wanasema wamechoshwa na kutangaziwa miradi hewa.
Vipindi kuhusu BIG RESULTS NOW vitaanza kurushwa kupitia redio za kanda ya ziwa ikiwamo Radio yangu Kasibante fm kuanzia ijumaa wiki hii, sikiliza mawazo ya wananchi na viongozi wao ana kwa ana.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment