maiti katika hospitali moja mjini
Naivasha umbali wa kilomita tisini kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Jamaa huyo anaitwa Paul
Mburu ana umri wa miaka 24 ambapo alipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya
kunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai kutokana na ugomvi wa kifamilia na babake
ingawa ilisemekana jamaa alifariki Jumatano usiku wakati akipokea
matibabu.
Wafanyakazi wa hospitali
hiyo walipigwa na butwaa na wengine kukimbia walipoona mwili wa mtu
aliyedhaniwa kufariki ukitembea na kuonyesha dalili za kuwa hai katika chumba
cha kuhifadhia maiti.
Afisa mkuu wa matibabu
katika hospitali hiyo ya wilaya Dokta Joseph Mburu amesema kuwa dawa
iliyotumiwa kumtibu Mburu hufanya moyo kupiga polepole hali ambayo huenda
ilimfanya muuguzi kudhani kuwa mgonjwa alikua amefariki.
Raia huyo wa Kenya
alisikika akimtaka mmoja wa wafanyakazi katika chumba cha kuhifadhia maiti
kumsaidia kwani alikuwa anahisi baridi kali na hapo ndipo mmoja wa wafanyakazi
alipotimua mbio kwa hofu.
Ndugu wa jamaa huyo
akiwemo babake walikuwa wametembelea chumba cha kuhifadhia maiti siku ya
Alhamisi ili kuanza kwa taratibu za mazishi lakini baadaye mchana
walifahamishwa kuwa Mburu alikuwa hai.
Mgonjwa anaendelea kupokea
matibabu katika hospitali ya Naivasha.
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment