MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Sunday, 12 January 2014

KIFO CHA WAZIRI MKUU WA IZRAEL

Alipatwa na Kiharusi Januari mwaka 2006 na tangu hapo akawa anatumia mashini kupumua. Hatimaye viungo vya mwili wa Sharon vimekuwa vikiathirika kutokana na hali yake mahututi.
 
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.

Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea kuwahudumia watu wa Israel.

Rais Shimon Peres, mwandani mkuu wa Sharon japo alikuwa hasimu wake wa kisiasa aliyejiunga na serikali ya Muungano na Sharon mwaka 2001, alisema Sharon alikuwa mtu mwema aliyepigania watu wake na kuwapenda na kuwa watu pia walimpenda.

Wadhifa wa Sharon kama waziri mkuu ulifika kikomo baada ya kupatwa na kiharusi na kisha kuwa katika hali mahututi kwa miaka minane tangu mwaka 2006.

Wakati huu wote alikuwa anatumia mashine kupumua na mirija kulishwa chakula.
Kabla ya hali ya Sharon kuzorota aliongoza jeshi la Israel kuondoka katika ukanda wa Gaza ili kupunguza taharuki kati ya Israel na Palestina.

MWANA HARAKATI

No comments: