MAC PRODUCTION STUDIO'S

MAC PRODUCTION STUDIO'S
KWA MATANGAZO YA BIASHARA REDIONI( 0767-814844)

Saturday, 18 January 2014

ASKARI MAGEREZA ASHIKILIWA NA POLISI KWA WIZI.

Jeshi la polisi visiwani Zanzibar linamshikilia askari wa chuo ch mafunzo Zanzibar ambaye ni sawa na askari magereza kwa tanzania bara, Sagin MEJA HASSAN IDDI (45) kwa tuhuma za wizi wa sh 1,635,000 alizoziiba kutoka duka moja lilipo eneo la Makadara mjini Zanzibar.

Afisa mkuu wa polisi Zanziba Inspekta Mohammed Mhina, amesema tukio hilo limetokea jana wakati askari huyo amevaa kiraia,alipofika dukani kama mteja wakati muuzaji akihudumia wengine, ndipo aliingia ndani na kufungua droo na kuchukua kiasi hicho, kisha kukimbia.

Amesema kuwa hatahivyo alikamatwa na polisi baada ya kufukuzwa na wananchi na kukutwa na fedha zote alizoiba.

Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoa wa mjini magharaibi Zanzibar ACP Mkadam Khamis Mkadam, amesema fedha hizo zilizokutwa mikononi mwa askari huyo, zimehifadhiwa ili kiwe kielelezo mahakamani, ambapo amesema ni tukio la tatu kutokea Zanzibar katika mwaka huu pekee, kwani kuna tukio lilitokea kwenye magahala ya Bakhresa na watuhumiwa watatu wanashikiliwa na walikuwa na silaha inayotumia risasi za shot gun.

Tukio lingine walikamatwa majambazi wanne akiwamo afisa wa TAKUKURU wakiwa na slaha 3 ikiwamo bastola na SMG  moja  walipomvamia mfanyabiashara mmoja na kumpora mili11.5.

MWANA HARAKATI

No comments: