Wapo waliowekeana dau kuwa CAG itamsafisha meya kutokana tuhuma, wengine wakisema kuwa lazima atiwe hatiani lakini baada ya ukweli kudhiilika waliowengi katika upande wake sasa wamemkana adharani wakiofiwa kupelekwa mahakamani, kutokana na madai ya bilioni zaidi ya mbili zisizojulikana zilipo katika mchakato wa kupitisha miradi ya maendeleo ya manispaa ya Bukoba.
Picha hii katikati ni aliyekuwa meya wa zamani wa manispaa ya Bukoba, Bwana Rwangisa, kushoto ni naibu meya wasasa Bwana Ngalinda ambaye sasa anashika mikoba kwa muda, na kulia ni katibu wa CCM wilaya Bukoba mjini.
Baada ya CAG kumaliza kazi yake, naibu waziri wa TAMISEMI AGREY MWANRI alifikisha ujumbe wa waziri mkuu PINDA kumtaka meya kujipima mwenyewqe kujiuzulu mara moja, jambo ambalo AMANI alisema alipopewa nafasi kuwa amekubali kutekeleza amri ya serikali.
No comments:
Post a Comment