WATU wasiofahamika
wamefukua kaburi la Rosa Kikwe, aliyefariki dunia mwaka 2005 na kuchukua mfupa
wake wa uti wa mgongo, kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Jeshi la Polisi Wilaya ya Bunda, limethibitisha kutokea kwa tukio hilo
lililotokea juzi, katika Kijiji cha Kihumbu, Kata ya Hunyari. Ilielezwa usiku
wa tukio hilo, watu hao walifukua kaburi alimozikwa mwanamke huyo, bila ya
ndugu wa marehemu kuwa na taarifa yoyote. Ofisa mmoja wa polisi, ambaye
hakupenda kutaja jina lake kwa sababu si msemaji, alisema baada ya watu hao
kuchukua kiungo hicho, walilifukia tena kaburi hilo na kisha wakatokomea
kusikojulikana.“Watu wasiofahamika walifukua kaburi la mwanamke huyo
aliyefariki dunia mwaka 2005 na kuchukua...
MWANA HARAKATI
No comments:
Post a Comment